Swahili News
- Je, uhalifu mashariki mwa Kongo ni "mauaji ya kimbari" ? April 2, 2025Mjadala kuhusu mada hii unafanyika mjini Kinshasa. Baadhi ya wataalamu, hata hivyo, wana shaka, wakiamini kwamba vigezo fulani lazima vizingatiwe ili kuzungumza juu ya "mauaji ya kimbari."
- Uingereza yasema haiungi mkono mpango wa Israel kwa Gaza April 2, 2025Naibu waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Hamish Falconer, amesema leo kuwa nchi hiyo haiungi mkono mpango wa Israel wa kupanua operesheni zake za kijeshi katika ukanda wa Gaza.
- Kenya yabadilisha kauli kuhusu mazungumzo yake na China April 2, 2025Kenya imekanusha kwamba ilijadili mpangilio mpya wa madeni na waziri wa fedha wa China baada ya kurekebisha chapisho kwenye mtandao wa kijamii .
- Baraza la Usalama la UN kuchukuwa hatua kali dhidi ya Kongo April 2, 2025Balozi wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa Jerome Bonnafont, amesema Umoja huo utaendelea kuchukua hatua kali dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
- Bardella: Maandamano yaliopangwa sio njama dhidi ya mahakama April 2, 2025Kiongozi wa chama cha National Rally cha Marine Le Pen, Jordan Bardella, amekanusha nia ya kuishinikiza mahakama ya Ufaransa kwa maandamano ya kumuunga mkono kiongozi huyo mkongwe wa siasa kali za mrengo wa kulia.
- Israel inatanua operesheni Gaza ili kuteka 'maeneo makubwa' April 2, 2025Israel imesema operesheni yake ya kijeshi katika Ukanda wa Gaza inatanuliwa ili kuyakamata maeneo makubwa, wakati maafisa wakisema kuwa mashambulizi ya usiku kucha ya Israel yamewauwa zaidi ya watu 40, wakiwemo watoto.
- Uhumimu wa msaada wa jamii kwa wagonjwa wa usonji April 2, 2025Maadhimisho ya siku ya uelewa kuhusu ugonjwa wa Usonji duniani, Umoja wa Mataifa unalenga jamii kutambua mchango wa kimaendeleo wa watu wenye ugonjwa huo.
- Kampuni za China zahimizwa kuheshimu sheria za nchi zilizoko April 2, 2025Ubalozi wa China mjini Bangkok, Thailand, umetoa wito kwa kampuni za China zinazofanya kazi katika mataifa ya nje, kufuata sheria za ndani za nchi hizo.
- Israel yasema jeshi lake linapanua operesheni zake Gaza April 2, 2025Waziri wa ulinzi wa Israel, Israel Katz, amesema kuwa operesheni ya kijeshi ya Israel katika Ukanda wa Gaza inazidi kupanuka ili kukamata maeneo makubwa ambayo yataongezwa kwenye maeneo ya kiusalama ya Israel.
- Kongo na waasi wa M23 kuanza mazungumzo ya ana kwa ana April 2, 2025Duru za pande hasimu nchini Kongo zimesema serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na waasi wa M23 wanajiandaa kwa mazungumzo ya ana kwa ana April 9.
- Marekani kuanza utekelezaji wa "ushuru wa kulipiza" April 2, 2025Marekani inatazamiwa kuanza kutekeleza leo amri ya Rais Donald Trump ya kuweka viwango sawa vya ushuru na ule unaotozwa na mataifa mengine duniani kwa bidhaa zinazotoka Marekani.
- Iran: Hatutakuwa na chaguo ila kutumia silaha za nyukliaer April 1, 2025Iran imesema haitakuwa na njia nyingine ila kutumia silaha za nyuklia endapo itashambuliwa na Marekani au washirika wake. Hayo ni kufutia kitisho chj rais wa Marekani Donald Trump aliyesrma ataishambulia Iran kijeshi.
- Bunge: Mpango wa kutokomeza umasikini Rwanda upitiwe upya April 1, 2025Bunge la Rwanda limeitaka serikali kufikiria upya sera yake ya kupambana na umaskini miongoni mwa wananchi, kwa sababu sera iliyopo inaonekana kutozaa matunda hadi sasa.
- Mali, Burkina Faso, Niger zatangaza ushuru mpya April 1, 2025Mataifa jirani ya kanda ya Sahel magharibi mwa Afrika ya Mali, Burkina Faso na Niger yametangaza kuweka ushuru wa pamoja wa asilimia 0.5 kwa bidhaa zote zinazoagizwa kutoka nje. Ushuru huo hautahusisha misaada ya kiutu.
- Hezbollah yasema haitaki vita na Israel April 1, 2025Afisa wa ngazi ya juu wa Hezbollah, Ali Ammar amesema kundi hilo halitaki vita na Israel, lakini liko tayari kupigana ikiwa vitaanzishwa.