Swahili News
- Umoja wa Ulaya na Uingereza ziongeza msaada wa kijeshi kwa Ukraine wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru. August 24, 2026Viongozi wa Ulaya, akiwemo Waziri Mkuu wa Uingereza Andy Burnham, wamekusanyika mjini Kyiv kuadhimisha miaka 35 ya Uhuru wa Ukraine.
- Zelensky: Ukraine yataka amani lakini haitasalimu amri August 24, 2026Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amesema nchi yake inataka amani, lakini haitasalimu amri kwa Urusi kwa gharama yoyote.
- Zambia yafunga mahakama siku ya mwisho ya kupinga uchaguzi August 24, 2026Mamlaka nchini Zambia zimefunga mahakama kuu za juu, na kuzuia watu kuingia katika majengo hayo, ambayo ni siku ya mwisho kwa upinzani kuwasilisha malalamiko ya kupinga matokeo ya uchaguzi.
- Ujumbe maalum wafuatilia usitishaji mapigano DRC August 24, 2026Ujumbe wa kwanza wa aina yake umetumwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kufuatilia utekelezaji wa usitishaji mapigano kati ya jeshi la serikali na kundi la waasi la M23, linaloungwa mkono na Rwanda.
- Watawala wa kiimla wanaozeeka Afrika: Mbinu mpya za kusalia madarakani August 24, 2026Nini hutokea watawala wenye nguvu wanapoanza kudhoofika? Viongozi kadhaa wa Afrika wanatumia mbinu tofauti kuimarisha mamlaka yao kwa muda mrefu, lakini haijulikani kama watafanikiwa.
- Eto’o amtetea hadharani Infantino August 24, 2026Nyota wa zamani wa Cameroon, Samuel Eto’o, amemtetea Rais wa FIFA Gianni Infantino, akisema “hakufanya kosa lolote,” licha ya shinikizo linaloongezeka la kutaka ajiuzulu.
- Syria yamfunga maisha Mufti Mkuu wa enzi ya Assad August 24, 2026Mahakama ya mjini Damascus imemhukumu kifungo cha maisha Mufti Mkuu wa zamani Ahmad Badreddine Hassoun kwa kuchochea ghasia za kidini, kuhalalisha mauaji na kutumia vibaya wadhifa wake.
- Miaka 60 ya ndoto, vikwazo na ukosoaji: Bwawa la Nyerere lakamilika August 24, 2026Kwa zaidi ya miaka 60 lilikuwa wazo lililopitia ukosefu wa fedha, ukosoaji wa wanamazingira na upinzani wa ndani na nje. Leo Tanzania imezindua Bwawa la Mwalimu Nyerere – ndoto iliyovuka vizazi vya viongozi hadi kutimia.
- Zelenskiy: Ukraine inataka amani lakini haitasalimu amri kwa Urusi August 24, 2026Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskiy, amesema nchi yake inataka amani, lakini haitakuwa tayari kujisalimisha kwa Urusi, akisisitiza msimamo huo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Ukraine.
- Miaka 35 ya uhuru: Ukraine yakataa amani ya kusalimisha ardhi August 24, 2026Ukraine inaadhimisha miaka 35 ya uhuru huku ikikabiliwa na mashambulizi makali, masharti ya Urusi na utegemezi mkubwa kwa washirika. Kyiv inasema inataka amani, lakini si kwa kusalimisha ardhi yake.
- Washirika wa Ukraine wakutana, ulinzi wa anga wadorora August 24, 2026Ukraine leo inaadhimisha siku ya uhuru, na imewakaribisha washirika wake wa Ulaya katika mkutano muhimu unaolenga kuongeza msaada wa ulinzi wa anga na shinikizo dhidi ya Moscow.
- Iran yapuuza shinikizo jipya la Marekani August 24, 2026Iran imepuuzilia mbali kampeni mpya ya Marekani ya kuongeza shinikizo la kiuchumi dhidi yake, ikisema hatua hiyo inapingana na madai ya Washington kwamba imeharibu uwezo wa kijeshi na nyuklia wa Tehran.
- Kwa nini makombora ya Urusi yanapenya ulinzi wa Ukraine? August 24, 2026Makombora ya balistiki ya Urusi yanaipa Ukraine muda mfupi mno wa kujibu. Uhaba wa mifumo ya Patriot na makombora yake unaacha miji mingi bila ulinzi wa kutosha.
- Baada ya vifo 518, tume mpya yasaka wahusika wa ghasia August 23, 2026Tume mpya ya Rais Samia imeanza kuchunguza wahusika wa ghasia za uchaguzi wa 2025, ikiwamo waliopanga, kufadhili na kuratibu matukio yaliyosababisha vifo vya watu 518. Wakati huo huo, kesi ya Lissu inaendelea mahakamani.
- Mkuu wa Jeshi Pakistan ajaribu kuyaokowa mazungumzo ya Iran August 23, 2026Mkuu wa majeshi wa Pakistan anatarajiwa kuwasili nchini Iran siku ya Jumatatu (Agosti 24) katika jitihada za kuzileta tena Tehran na Washington kwenye meza ya mazungumzo kukomesha vita dhidi ya Jamhuri hiyo ya Kiislamu.
